Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, June 28, 2013

MBUNGE SUGU AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

 
Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.CHANZO JFORAM
Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...