Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 3, 2013

MBUNGE MSIGWA ASHINDWA KUTOKEA MAHAKAMANI LEO

Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani hivi karibuni (picha na maktaba yetu )
............................................................................................
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) leo ameshindwa kufika mahakamani katika kesi yake na watuhumiwa wengine zaidi ya 90 wanaotuhumiwa kwa makosa matatu likiwemo la kufanya vurugu wakati wa mgogolo wa machinga kuvunja sheria katika eneo la mashine tatu .
Taarifa zilizotolewa mahakamani hapo leo zinadai kuwa mbunge Msigwa ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kuwepo Bungeni mjini Dodoma .
WAtuhumiwa katika kesi hiyo mbali ya mbunge Msigwa wengine ni pamoja na diwani wa kata ya Mvinjeni Bw Frank Nyalusi (chadema) na katibu mwenezi wa Chadema Iringa mjini Bw Joseph Mgimwa .

Akisoma kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Adolfu Maganda alisema kuwa
watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kuharibu gari la uokozi
na zima moto mali ya Manispaa lenye namba za usajili SM 9323.
kwa kupasua kioo cha mbele.
Vurugu hizo zilitokea Mei 19 mwaka huu baada ya mbunge huyo kufanya
mkutano wa hadhara katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoni na
kuamuru wafanyabiashara hao kuendelea kufanya biashara zao katika
eneo la mashine tatu eneo ambalo kisheria haliruhusiwi .

Mei 19 wafanyabiashara hao walifika katika eneo la mashine tatu na
kupanga bidhaa zao bila kujali amri ya kuwakataza kufanya biashara
katika eneo hilo jambo ambalo liliwalazimu Polisi wa kutuliza ghasia
(FFU kutumia nguvu ikiwamo kufyatua mabomu ya machozi,kutumia maji ya
kuwasha na kupiga risasi za moto kwa lengo la kuwatawanya machinga
hao.

Upande wa mashitaka umedai kuwa bado upelelezi wa shauri hilo
unaendelea na kwamba kesi hiyo itatajwa tena Juni 24 mwaka huu.
 
Credits: Matukio daima
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...