Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, June 12, 2013

Mama mwenye nyumba ampandishia kodi Denzel aliyekuwa mwakilishi wa Uganda katika BBA ‘The Chase’, sababu kamuona kwenye TV!

denzel2

Hakika jina la Denzel limeongezeka thamani na umaarufu pia Africa na nchini kwake Uganda, kiasi mpaka mama mwenye nyumba anayokaa kuamua kumpandishia kodi star huyo wa big brother pamoja na kwamba hakuweza kufika kilele cha safari ya kui ‘chase’ $300,000.

Denzel mwenye miaka 30 ambaye ni mtangazaji wa radio na TV huko Kampala, Uganda amejikuta akipata ongezeko la gharama za maisha baada ya mama mwenye nyumba wake kuamua kumpandishia kodi baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini. Denzel alipohoji kwanini ameamua kumpandishia kodi mama huyo alijibu kuwa anajua kuwa sasa Denzel ana hela sababu alikuwa anamuona kwenye TV South Africa.
Haya ndio maneno ya landlady huyo “Oh, I know you have money, I saw you on tv in South Africa”
Mtandao wa Uganda online umeripoti kwamba Denzel mwenye vituko na ucheshi amesema mama huyo amemuongezea kodi kiasi cha Ugx200,000/- ambayo ni sawa na USD 80 kwasababu tu kamuona kwenye runinga Afrika Kusini.
“After just two weeks out of my house. I come back and inform her I will be moving back in and she wanted to increase my house rent by a stunning 200k! (+/-USD 80!)” ailsema Denzel.
Kwakuwa mama wa watu kamuona Denzel kwenye TV South Africa huenda anajua kila anayetoka hupewa pesa!
Haya kwa wale wanaoutamani umaarufu chukueni hiyo, umaarufu bila hela ni mzigo wa mwiba! Ila ni mtazamo wangu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...