NA MWANDISHI WETU
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba (pichani)amesema
dhamira ya kuwepo kwa vyama vingi bado haijafikiwa tangu kuanzishwa
kwake kutokana na kukosa vyama na viongozi wenye dira kwa Taifa.
Aliyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wamnafunzi
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa
wa Dar es Salaam.
Makamba
ambaye pia ni Mlezi wa Vyuo Vikuu Tanzania alisema vyama hivyo
vimekuwa vikijikita katika kulalamika bila kuonyesha dira na mwelekeo
tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya fujo ambazo zinakwamisha
jitihada za serikali.
Makamba
alisema Serikali inafanya kazi kutokana na mipango yake ambayo
imejiwekea yenyewe hivyo inaamini kuwa itafikia malengo yake bila
kusukumwa na mtu.
“Kwa
kweli najuta kwanini tuliruhusu uwepo wa vyama vingi hapa nchini kwani
lengo letu lilikuwa ni kudumisha demokrasia kitu ambacho kimekuwa
kinyume kwani vyama na viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na
dhima ya lengo husika,” alisema
Naibu
Waziri alisema CCM ni chama ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa
hivyo wao wanaamini kuwa heshima hiyo itaendelea kuwepo milele kwa
milele.
Alisema
vijana wa CCM wahakikishe kuwa wanakisaidia chama na nchi kwa ujumla
ili nchi isije kuchukuliwa na vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa
na kuipeleka nchi kuzimu.
Aidha
Mlezi huyo aliwataka vijana hao wanaomaliza kujiamini na kuthubutu
kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza ili waweze kupata
urahisi wa kushiriki katika chama na serikali kwani ni wajibu wao
kulitumikia Taifa.
Makamba
alisema vijana wanapaswa kushiriki katika harakati za kisiasa kwani
hayupo mtu amnbaye atapata jambo bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana
na dhana ya kutafutiwa kazi kama wengi wanaofikiri.
Aliwataka
wingi wao uwe ni sehemu muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la
Tanzania ijao ikiwa ni kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na
kuondokana na dhana kuwa mwenye uwezo wa fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi
huyo alisema dhana ya fedha katika kutafuta uongozi ipo kwa baadhi ya
watu kutokana na tabia ya mtu mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia
kama kigezo.
Naibu
Waziri aliwataka vijana wa CCM kuondoa uoga katika maamuzi ambayo
yanahusu maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla iwapo sifa za uongozi
unazo.
Makamba
aliwaambia vijana kutambua kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na
kuachana na tabia ya kulalamika kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee
jambo ambalo wanalitengeneza wenyewe.
Aidha
aliwataka wasomi kutafuta maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu
Nyerere kwani yana msingi mkubwa katika kujitambua na kufanya maamuzi
sahihi kuhusu nchi yao na uongozi kwa ujumla.
Naye
Mwenyekiti Vyuo Vikuu Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari Asenga alisema
katika mahafal;i hayo wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28 vya
mkoa wa Dar es Salaam walishiriki katika sherehe hiyo.
Asenga
alisema huo ni uataratibu ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa
shirikisho hilo lengo likiwa ni kuwatambua na kuwapatia vyeti vya
utambulisho wao ndani ya CCM.
Alitaja vyuo ambavyo vilishiriki ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT, TSJ na vingine vingi.
Kwa
upande wa msoma risala kwa niaba ya wahitimu Innocent Nsena alisema
wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo
kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana na changamoto za jamii pamoja
na vyama vya upinzani hapa nchini.
Aidha
alisema wanavyuo wanapendekeza maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo
wanaomba nchi ya Tanzania kutokubali kuwa na serikali ya shirikisho
kwani uwezo wa nchi bado ni mdogo kuendesha nchi ambayo bado ni change
kuichumi.
Pia
wanapendekeza upatikanaji mpya wa kupata mgombea urais ili kuondoa
mpasuko ambao unatokea mara kwa mara baada ya uchaguzi kufanyika.
Alisema
katika mazingira yoyote yale Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana
na mazingira mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni
vyema wakatumia mfumo wa kujaza dodoso ili wana CCM wapendekeze Rais
wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.
Credit: Emmanuel Shilatu Blog