Waandamanaji nchini Misri
Raia wa
Misri wamefanya maandamano makubwa kote nchini kumshinikiza rais wa
taifa hilo Mohammed Morsi, kujiuzulu wakati wa maadhimisho yake ya
kwanza tangu achukue hatamu ya taifa hilo.
Ijapokuwa barabara za mji wa Cairo zina utulivu kufikia sasa, maafisa wa polisi wamewekwa katika kila sehemu ili kuzuia ghasia.
Wapinzani
wa rais huyo wanamkashifu kwa kushindwa kutatua maswala ya kimsingi
kama vile uchumi pamoja na usalama na kudai kuwa zaidi ya raia millioni
22 wametia sahihi ya kutaka uchaguzi mpya kufanyika mara moja.
Aidha
wanadai kuwa rais Morsi, ameweka ajenda ya Kiislamu ya chama chake cha
Muslim brotherhood mbele kushinda mahitaji ya raia wa taifa hilo.
Wafuasi wa rais huyo pia wameapa kufanya mikutano ya hadhara kumuunga mkono kiongozi wao.



