Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya L Hayat Investment
Limited ya nchini Oman, imetoa dola za kimarekani 10,000 ni sawa na
sh.milioni 15 za kitanzania, kwa ajili ya kudhamini shindano la urembo
la redd’s miss Tanga, linalotarajiwa kutimua vumbi Juni 22 kwenye Uwanja
wa mkwakwani.
Mkurugezi wa Kampuni ya DATK
Intertaimeint, Asha Kigundula, ambaye ndiye muandaaji wa shindano hilo,
alisema kuwa, amefurahi kupata kiasi hicho cha fedha kwa kuwa
kimemsaidia kwa asilimia kubwa kufanikisha shindano hilo.
Alisema kuwa kwa namna nyingine
anamshukuru .mkurugenzi wa kampuni hiyo Shekhe Salim Al Harthy kuweza
kumsaidia kiasi hicho. “Namshukuru sana mr Salim kwa. Kuweza kunisaidia
kama hivi, nina amini kila kitu kitakuwa kipp sawa”alisema Asha.
Katika hatua nyingine Asha
alisema, katika shindano hilo jaji anatarajiwa kuwa mwandishi wa
Freemedia inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari Clezencia
Tryphone ‘Tasha’ ambaye atasaidia kazi na Miss Tanzania miaka kadhaa
iliyopita ambaye yuko katika mazungumzo naye ya mwisho.
Aliwataja warembo hao kuwa ni Hawa
Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel
(18),Wahida Hashimu(20), Tatu Athumani (19), Mwanahamis Mashaka(20),
Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha
Rashid (21),Hzina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moreli (21) na
Hawa Twaybu(21)
Alisema kwamba shindano la mwaka
huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK
imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa
ujumla wakae mkao wa kupata raha na kudai kuwa burudani atazitangaza
katikati ya wiki hii.
Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa
na L Hayat Investment Limited, Dodoma Wine, CXC Africa,Executive
Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment
LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud’s Media Group,
pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna,
JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar blog



