Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, June 6, 2013

KENYA YATWAA UBIGWA NA KUING`ARISHA AFRIKA MASHARIKI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE


Ephantus Nyambura & Samuel Papa



 Mei 5 2013, Dar es salaam:  Haijawai kutokea mpambano mkali katika GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kama  uliooneshwa jana katika fainali za mchuano Pan-African Guinness Football Challenge kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV .
Fainaili ilikuwa na ushindani mkubwa  ambapo timu mbili kutoka Afrika Mashariki na nyingine mbili kutoka Afrika Magharibi zilichuana vikali kila timu zikiwania kupeleka ushindi nchini kwao. Ilikuwa ni zaidi ya kupeperusha bendera ya Kenya kwani nchi zote za Afrika Mashariki ziliwakilishwa na timu hiyo.
                                                                                                                    
Mchuano huo ulianza kwa shangwe katika raundi ya maswali na majibu ambapo Ephantus na Samuel kutoka Kenya walingara. Raundi ya kwanza iliisha timu moja kutoka Kenya ikiwa inaongoza na timu nyingine kutoka Kenya ikishika mkia, Francis na Kepha kutoka Kenya walikuwa wa kwanza kutolewa wakijishindia dola za kimarekani 4,500 tangu washiriki mashindano hayo.
 Wakiwa na presha kubwa timu moja kutoka Afrika Mashariki iliyobakia (Ephantus na Samuel) ilionesha jitihada zake kubwa za kutowaangusha wana Afrika mashariki kwani walijua fika kwamba si Kenya pekee inayowategemea bali Tanzania na Uganda zimeelekeza macho yao katika timu hiyo.
Kuelekea katika raundi ya pili, je timu mbili kutoka Ghana zitaifungisha virago timu ya Kenya na kuifanya Afrika Magharibi kuingiiza timu zote katika hatua inayofata? Akiwa katika jezi ya bluu Jonathan kutoka Ghana alimudu  maswali  lakini kwa mara nyingine timu kutoka Kenya ilimkabili vyema na kurudisha mashambulizi. Mwisho wa mchuano wa raundi hiyo Jonathan na Desmond  kutoka Ghana waliaga mashindano wakiwa na kitita cha dola 25,000.
Bara liligawanishwa vilivyo baada ya timu ya Kenya (Ephantus na Samuel) kutoka Afrika Mashariki na timu ya Ghana (Emmanuel na Isaac) kutoka Afrika Magharibi kuingia katika hatua ya penati. Timu hizi zilikutana wiki iliyopita katika nusu fainali na sasa ni timu ipi itatwaa ushindi na kuipeperusha bendera ya nchi yake?
Pamoja na kushindwa wiki iliyopita, Ephantus na Samuel kutoka Kenya kwa ujasiri mkubwa na uwezo mkubwa waliouonesha jana waliweza kuwashinda waghana na kujipatia nafasi ya kufika hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Emmanuel na Isaac kutoka Ghana waliikosa nafasi ya ukuta wa pesa wa Guinness  ila waliondoka kwa furaha huku wakijivunia kuwa timu bora kutoka Afrika Magharibi  huku wakiwa na kitita cha dola za kimarekani  9,000 mfukoni.
Ephantus na Samuel walithibitisha uwezo wao kwa kupiga `target four’ katika ukuta wa pesa wa  Guinness na kuwafanya wajishindie dola za kimarekani 12,000.
“Kampuni ya bia ya Serengeti inatoa pongezi kubwa kwa Ephantus na Samuel!  Kwani hawakuipeperusha bendera ya Kenya pekee bali  wameiwakilisha Afrika Mashariki kwa  ujumla. Hongereni sana! Tumekuwa tukitazama mashindano haya kwa wiki 12 kupitia televisheni za ITV na Clouds TV  na tumeona timu mbalimbali kutoka Afrika zikichuana kuwania ushindi wa GUINNES FOOTBALL CHALLENGE  lakini kwa uwezo mkubwa waliotuonesha, ushindi umebaki kwetu Afrika mashariki “. alisema Meneja wa bia ya  Guinness Davis Kambi.
Mashabiki wetu wanaweza kuendelea kushiriki mchezo huu wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kupitia simu zao na kujipima uwezo wao katika mchezo huu. Jiunge bure kupitia m.guinnessvip.com na uone uwezo wako katika kuiwakilisha nchi yako.
 Hakikisha unatembelea ukurasa wetu  wa Facebook
Tafadhali kunywa kistaarabu.  Ni maalumu kwa 18+
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...