Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Tuesday, June 4, 2013

JAMAA WAPIGA SHOW MOROGORO BILA KUJALI MSIBA WA NGWEA, AFANDE SELE KAFUNGUKA YAKE

IMG_1447 
Afande Sele akiwa na shemeji yake msibani

    Kufuatia kifo cha Albert Mangwea kilichotokea Afrika kusini na mazishi yakiwa bado hayajafanyika. Wasanii wengi walisitisha show zao, lakini kituo cha Radio cha mjini Morogoro Planet fm walishindwa kusitisha show yao ambayo imefanyika j.mosi katika ukumbi wa Tanzanite Complex. 
  
   Baadhi ya wadau wamelaani kitendo hicho kwa kukiita si cha kibinaadamu wakati ukizingatia show zenyewe ninategemea wasanii kama hao.
   Kwa upande wake msanii maarufu na Mfalme wa Rhymes Tanzania Mfalme Sele ameamua kuyasema yake ya moyoni juu ya kitendo hicho cha kinyama

     
Msipokuwa wa kweli kwa kumshauri Fredi, radio yenu itakuwa na siku chache sana kuwepo hai kwa kuwa radio yeyote inatemegemea watu na watu ni walewale "wanaokwenda harusini ndio haohao wanaokwenda msibani" msiba wa Mangwea umemgusa kila mdau wa muziki hasa vijana nyinyi kama radio/ukumbi (wadau wa burudani) mnawaitaji na kuwategemea sana vijana katika kazi zenu, kila msanii, kampuni zinazodili na vijana walihairisha show zao Nchi nzima ili kuenzi na kuonyesha heshima kwa Ngwea/Bongofleva kasoro nyinyi PLANET FM tu, huo sio uungwana wala utu na zaidi ukizingatia Ngwea ni mtoto wa Morogoro na Mazishi yake yanafanyika hapa Morogoro, mlichokifanya nyinyi PLANET FM ya morogoro ni sawa na matukio mawili katika nyumba moja, yani nyumba hiyo hiyo moja (Moro) ina msiba halafu nyinyi mkaweka harusi pia uliona wapi kama si uchuro, dhambi na matusi? Mimi ningewezaje kuja ukumbini wakati ndio nasimama kama mwenyeji wa wasanii na wadau wote wa burudani hapa Moro? Ningeelewekaje kama King wa Bongo Flavour na hata watu wa Moro wangaenionaje kama ningefanya show yenu ya jumamosi? Wanaokushangilia leo ndio hao hao watakaokupiga mawe (watakuzomea) kesho kama ukiwakosea, msipojitazama watu wanaweza kususia radio mpaka ukumbi wenu kwa kuangalia pesa bila kujal utu, mfano ningekufa mimi Selemani, Mhando, Warda, Fredi, Zombi, Frado n.k mngefanyaje hiyo show yenu? Je sisi tunathamani kuliko Ngwea katika tasnia ya muziki wa bongofleva? Sasa mitandao, radio, Tv, magazeti yakianza kuwachafua PLANET FM kwa kitendo hicho mtapona? Hayo makampuni yatawapa tena matangazo na ukumbi wenu watu wataendelea kuutumia kwa show? Mmesahau kuwa Moro wameshawai kususia kila kitu cha Abood kuanzia mabasi, tv, radio n.k, kwa kutojali kwake utu na kuangalia pesa tu? Mimi sikufika ukumbini nimefiwa kwa kujali utu, kulinda heshima yangu, yenu na Moro kwa ujumla sasa kama hamkunielewa mtakuwa mmechelewa sana na NINAAMINI HILI JAMBO HALITAPITA KIMYAKIMYA BILA MITAA KUJUA UKWELI. Team amani na upendo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...