"Njia
ya Obama kuelekea kwenye kushinda tuzo hiyo ya juu kabisa haikuwa
rahisi. Na moja ya anguko la Obama la njiani ni pale, kama wasemavyo
Waswahili, ‘alipogalagazwa’ na Mmarekani mweusi, Mzee Bobby Rush. Ni
mwaka 2000, kwenye Uchaguzi wa kuingia kwenye Baraza la Halmashauri kule
Chicago. Obama , akiwa kijana na msomi wa Chuo Kikuu alipambana na
mzoefu wa siasa, Mzee Rush, na kilichomtokea ni kuambulia kura chache.
Obama hakuwa mzoefu kwenye
mijadala. Aliongea kisomi zaidi, na hadhira yake haikumwelewa. Wakati
Mzee Rush alikuwa mzoefu wa siasa, na aliongea lugha ya watu, Mzee Rush
alilimudu sana jukwaa. Obama alipotakiwa kutoa maoni yake baada ya
anguko lile alitamka;
“ Kwangu kilichonitokea ni kama
kupata ‘Elimu ya Siasa’!” Anasema Obama. Ni hapo, ndipo Obama alipoanza
kujifunza zaidi misingi ya kushindwa, kusimama, na kuendelea kupambana,
na hatimaye kushinda, na zaidi, kujifunza kutokana na kushindwa."
Maggid,
Iringa.



