Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao
baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na
wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo imefanyika kwenye Taasisi ya Mara
Foundation ya jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”
Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika
baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa
semina hiyo.
Pichani
juu na chini ni Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny”
wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha
iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo
pichani).
Mwendeshaji
wa Semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akigawa kitabu
chake kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa "Nayakumbuka
Yote" ambacho kinauzwa katika maduka mbalimbali ya vitabu jijini Dar na
Pesa inayopatikana katika mauzo hayo asilimia 80 inakwenda kulipia ada
za shule kwa wasichana ambao ni mayatima na asilimia 20 inakwenda kwa
mchapishaji.
Mmoja
wa washiriki akimpongeza Hoyce Temu kwa ujasiri aliokuwa nao na mateso
aliyopitia katika maisha yake mpaka kufikia hapo alipo.
Hoyce Temu akisaini autograph kwa mmoja washiriki.
Hoyce Temu akishow love na Mmiliki wa Beutylicious Saloon iliyopo Mikocheni B Irene Juliet Mbuya.
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya washiriki wakipata picha ya ukumbusho na
Mrembo wa zamani aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1999
Hoyce Temu.
Vijana
jijini Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki katika semina
iliyoandaliwa na Mikono Business Consult kwa ajili ya kuwapa hamasa na
kuwataka wasikate tamaa ili wajipange na kuangalia nini wanachotaka
kukifanya katika maisha yao.
Semina
hiyo iliyoendeshwa na Miss Tanzania wa zamani na Communication Analyst
wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu ilifahamika kwa jina la “How
To Find Your Destiny” imeonekana kuwavutia washiriki waliohudhuria
kutoka sehemu mbalimbali.