Mwanafunza wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma
aliyekuwa akisoma mwaka wa pili (Diploma in Business Administration) Bw.
Frank ndakidemi jana Tarehe 09/06/2013 siku ya Jumapili alifariki Dunia
kwa ajali ya pikipiki wakati akitokea maeneo ya Area D (barabara ya
njia panda Area D). Hata vivyo ajali hiyo ilitokea Asubuhi sana mnamo
saa 12 ,wakati Marehemu alipokuwa akiendesha pikipiki na kisha kugongana
na gari aina ya Hiace. Hata hivyo ajali hiyo ilimpelekea kuumia vibaya
maeneo mbalimbali ya mwili hatua iloyosababisha apoteze maisha,kufuatia
ajali hiyo jeshi la Polisi limeendelea kuchunguza chanzo cha ajali
hiyo. Aidha mwili wake ulihifadhiwa katika Hospital kuu ya mkoa wa
Dodoma ili kusubiri taratibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua ya
kusafirisha Mwili huo. Katika hatua nyingine Marehemu alipata ajali
akiwa amempakia rafiki yake(jina lake halikupatikana mara moja) ambaye
kwa upande wake aliumia na amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma
Wodi namba kumi,ambapo anaendelea na matibabu. Akizungumza na chanzo
chetu cha Habari Mshauri wa wanafunzi wa CBE Bw. Sikato amesema "Mwili
wa marehemu unatarajiwa kuagwa leo chuoni hapo ikiwa ni baada ya mzazi
wa(Baba) kuwasili jana usiku akitokea Iringa ,kisha Mwili huo
unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Moshi ambapo hatua mbalimbali ikiwemo
mazishi zitafanyika" Kwa hakika Musiba huu uliibua simanzi sana kwa
wanafunzi wote wa CBE. Akizungumza na chanzo chetu cha habari
Bw.Remidius Emmanuel (Aliyekua kiongozi wa COBESO) Amewataka wanafunzi
wote wa CBE kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na kuzidi
kumuomba MUNGU ili kuwa wastahimilivu wa matukio kama haya, Hakika hii
ni safari ya kila mmoja wetu ila mwenzetu katangulia, Alisema Bw.
Remidius" |