Baadhi ya ndugu na marafiki wa Mtanzania aliehukumiwa kifungo cha miaka
nane nchini Angola baada ya kupatikana na dawa za kulevya alizokua
akizisafirisha kwenda Afrika Kusini, wamepaza sauti kuomba msaada wa
Serikali ili ndugu yao aje kufungiwa gerezani Tanzania.
Khaleed Bin Abad amesema huyu Mtanzania aliondoka South Afrika na kwenda
kufata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukua ila wakati
anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na
kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.
Kwa kipindi chote hicho huyu jamaa amekua akishikiliwa Angola bila kujua
hatma yake na hata kushindwa kukutana na balozi wa Tanzania Angola
lakini wiki mbili zilizopita ndio amehukumiwa kifungo cha miaka 8.
Ombi lililoambatana na ndugu hawa kupaza sauti, ni kuiomba serikali
kusaidia mtu huyu kukutana na balozi wa huko ili utaratibu wa kuja
kufungwa Tanzania ujulikane.
Mara nyingi Mtanzania huyu amekua akituma msg kwa kutumia simu za watu wengine aliokutana nao gerezani.
VIA MILLARD.