Wafanyabiashara
maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na
Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la
kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 1WAZIRI
Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu
kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza
katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu
mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.
Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.
“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji
kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni
cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.
Lowassa alisema tatizo la
ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana
kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.
“Ndiyo maana CCM katika ilani
yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake
vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.



