Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 3, 2013

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHATOA NASAHA KWA VIJANA ARUSHA

DSC01074
Mahmoud Ahmad Arusha
Chama cha wananchi(CUF)kimewataka na kuwanasihi vijana kote nchi kujadili uzalendo wao kwa nchi yao na kuacha kushabikia siasa kwani siasa ndio maisha yao na wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vibaya kwa manufaa yao binafsi bila ya kujali kesho yao.
Kauli hiyo imetolewa kwenye muendelezo wa kampeni ya udiwani wa kata ya Elerai na mkurugenzi wa habari na uchaguzi wa CUF Abdul Kambaya wakati akimnadi Mgombea udiwani wa CUF John Bayo kwenye kata hiyo.
Kambaya aliwataka wakazi wakata ya Elerai na kata zote ambazo uchaguzi mdogo unafanyika kuwachagua wagombea wa chama hicho kwani wananchi hao hawatajuta kuwachagua wagombea wa chama hicho.
Aliwataka vijana kuacha kufanya vurugu kwenye kampeni kwani wanaowatuma hawatawasaidia na kubaki kuwasumbua wazazi wao na jamaa ambao maisha yetu teyari yapo kwenye wakati mgumu wa kipato na kiuchumi  nawasihi kuacha kutumika kwa faida ya wana siasa uchwara ambao wapo kwa maslahi binafsi.
“siasa zetu tunazozifanya zisitugombanishe wala kutugawa kwa udini ukabila,ukanda na itikadi za vyama tujadili maisha na mustakabali wa maisha ya watanzania na tutawafanyia nini mkituchagua hao wanaofanya matusi na vurugu msiwape kura kwani hawaitakii mema nchi yetu”alisema Kambaya
Kambaya aliwataka vijana kujadili mustakabali wa maisha yao zikiwemo fursa za matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hapa nchi leo vijana wamejikita kwenye kazi ya boda boda wakati huu ukiwauliza kazi gani wanataka kufanya watakwambia kuendesha bodaboda huu ndio mfumo wa elimu ambao haumwandai mwananchi kijana kufika kwenye kuwa na utaalamu wakati akimaliza masomo.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa chama hicho kata ya Elerai John Bayo alisema kuwa hakupewa wala hakuchaguliwa na wimbi la mafuriko ya chadema bali ni wananchi wa kata hiyo ndiyo mlinipa kura kwenda kuwatumikia kwenye vikao vya halmashauri hivyo nawaombeni muwaonyeshe hao kuwa mimi ndiyo chaguo lenu.
Bayo ukiona mtu anatukana ujue kakosa sera ya kuongea na mtu kama huyo muogopeni kama ukoma sisi wakazi wa Arusha hatuendeshwi na mawazo ya mtu mmoja sasa nawaombeni mumuonyeshe kuwa Arusha ina wenyewe Je wakazi wa Arusha mliotuchagua mlikuja kuulizwa kama sisi hatufai kwani nyinyi ndio mliotupa kura si chadema hapo mmeonae

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...