Penny akiwa hospitali.
TUMEINYAKA
kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’,
inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda
linashuka nayo.
Habari
zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu
wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa
kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha akalazwa,
akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.
Diamond na Penny katika pozi.
Akizungumzia hali hiyo,
kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na
mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.