HAUSIGELI
ambaye jina lake halikupatikana mara moja, nusura ajirushe chini kutoka
ghorofa ya pili kwa kile kilichodaiwa kuwa aliogopa moto mkubwa
uliozuka katika jengo la jirani na ghorofa alilokuwemo.
Tukio hilo lilijiri mapema
asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na
Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa majirani, baada
ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye
jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha
chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo.
Alifanikiwa kukaa kwenye
sehemu ya ukingo wa ghorofa hilo na kujiandaa kwa tukio la kwenda chini
akiamini atakuwa amejiokoa na moto huo.
Hata hivyo, bosi wa hausigeli
huyo alipoona zoezi hilo la hatari alitoa mkono dirishani na kumvutia
ndani mfanyakazi wake huyo tukio ambalo lilijiri muda mfupi kabla ya
Kikosi cha Zima Moto kufika na kufanikiwa kuuzima bila kujeruhi mtu.
Source:GPL