![]() |
| Picha zote hazihusiani na ajali hiyo ya Uganda |
![]() |
WATU
29 wameripotiwa kufa nchini Uganda na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa
vibaya na moto uliotokana na ajali ya lori la mafuta lililoanguka.
Habari
kutoka Uganda zinasema ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea katika
barabara kuu ya jijini Kampala na kwamba zaidi ya pikipiki 20 nazo
ziliungua kwenye tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la Polisi
nchiini humo.
Inaelezwa
kuwa mara lori hilo lilipoanguka wakazi wa jijini hilo walilivamia kwa
nia ya kuzoa mafuta kabla ya kutokea mlipuko uliowaunguza watu hao ambao
baadhi walikimbilia kwenye madimbwi ya maji ili kupoza machungu ya moto
na kupotea uhai wao na kuopolewa kwenye maji.
Zaidi
ya watui 2o wameripiwa kukimbizwa hospitalini wakiwa hoi kwa kujeruhiwa
na moto huo ambapo unaelezwa ulianzishwa na mmoja wa wahanga hao wakati
wakimbilia kwenye ajali hiyo bila kujua lori lilikuwa limerbeba
petroli.





