Mshindi
wa Redd's Dar City Center, Alice Isack (katikati) akipunga mkono kwa
furaha, akiwa na mshindi wa pili, Clarah Paul (kulia) na mshindi wa
tatu, Fatma Hussein (kushoto) baada ya kutangazwa washindi katika
shindano lililofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar Es
Salaam jana.
Miss Tanzania 2012, 2013, Brigt Alfred (wa pili kushoto) Miss Tanzania 1997, Hoyce Temu (kushoto) wakifurahia shindano hilo.
Wema Sepetu (katikati) akiwa ni miongoni mwa walioshuhudia shindano hilo jana usiku.
Meneja
wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro akifuatilia kwa umakini
shindano la Redd's Miss Dar City Centre jijini Dar Es Salaam jana
usiku.
Sehemu ya mashabiki wa Tasnia ya Urembo wakishangilia matokeo ukumbini humo.
Burudani jukwaani wakati wa shindano hilo.
Warembo waliofanikiwa kutinga hatua ya tano bora, baada ya kutangazwa.
Hoyce Temu (kulia) akiwauliza maswali warembo waliofanikiwa kutinga hatua ya tano bora.
Warembo watatu bora wakiwa na zawadi zao za mfano wa hundi kila mmoja baada ya kutangazwa washindi na kukabidhiwa.