Mtuhumiwa akihojiwa na polisi
MWANAMUME aitwaye Andrew Kabula (34), mkazi wa Kimara Mwisho jijini,
hivi karibuni alinaswa gesti akiwa na mwanafunzi ‘denti’ aliyetaka
kufanya naye ngono ili ampatie kazi bandarini..
Kabula a.k.a Afisa Feki alijitapa kwa denti huyo kwamba ni Afisa wa
Mamlaka ya Bandari jijini Dar na ana uwezo wa kumpatia kazi kama atampa
rushwa ya ngono.
Kwa kutambua kwamba kitendo hicho ni kosa kisheria, denti huyo (jina
lake kapuni) aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu ili kumnasa afisa
huyo feki.
Waandishi wetu waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbezi Luis jijini
Dar na kumwekea mtego jamaa huyo katika gesti aliyoichagua, iliyopo
maeneo ya Kimara jijini Dar.
Afisa huyo kila mara alikuwa akiwasiliana na denti huku akimsisitiza kutoondoka hapo kama kweli alitaka ajira.
Waandishi, askari na denti walitangulia katika gesti hiyo na afisa akataarifiwa na denti kwamba ameshafika eneo la tukio.
Yakafuata maelekezo ya kuchukua chumba kutoka kwa afisa huyo aliyedai kwamba yupo mbali kidogo.
Saa moja usiku, afisa feki alifika katika eneo la tukio na kuingia
chumbani katika gesti hiyo (jina tunalo), huku askari na waandishi
wakifuatilia nyendo zake.
Bila ya kushtuka kama amewekewa mtego, moja kwa moja afisa aliingia
chumbani na kumkuta denti huyo ambaye alizidi kumsisitizia lengo lake.
Baada ya kuhakikishiwa kile anachokitaka na denti huyo, afisa alisaula viwalo vyake vyote na kuwa tayari kwa tendo.
Denti aliendelea kujibaraguza na kutuma taarifa kwa askari na waandishi
wetu kwamba jamaa alikuwa tayari kwa tendo ndipo timu nzima ikavamia
chumbani
Mara baada ya askari kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi, afisa huyo
alipekuliwa katika simu yake ya kiganjani na kukutwa na meseji kadhaa
zikionesha kwamba alikuwa akifanya mawasiliano na wasichana wengi kwa
ajili ya kuwapa kazi bandarini.
Katika kudhihirisha kuwa ni tapeli mzoefu, siku hiyohiyo afisa huyo
alikuwa na ahadi na msichana mwingine ambaye katika simu jina lake
‘liliseviwa’ kwa jina la Mariam ili apewe rushwa ya ngono.
Inadaiwa kwamba, tapeli huyo amekuwa akiwadhalilisha wasichana wengi kwa
staili yake hiyo ya kuwadanganya kuwapatia kazi na kisha kuwaacha bila
ya ajira.
Baada kutiwa nguvuni na kupelekwa Kituo cha Polisi, ilibainika kwamba
jamaa si mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari bali ni deiwaka wa udereva wa
daladala zinazofanya safari zake kati ya Ubungo na Msata mkoani Pwani.
Katika kuonesha jamaa ni mtata, alipofikishwa kituoni na baada ya
kuandikisha maelezo alisema kwamba alikuwa akihitaji selo ya peke yake
kwani hataki kuchanganyika na watu.
Credit: GPL