Katika
mchango wake, Keisy alisema haungi mkono hoja kwa sababu Barabara ya
Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha
lami.
Pia alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Pia alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Mara
baada ya Bunge kuahirishwa, Keisy akiwa nje ya ukumbi huo alifuatwa na
Mbunge wa Urambo Mashariki, Profesa Juma Kapuya, Omary Nundu (Tanga
Mjini), Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na Rita Kabati (Viti Maalumu)
na kumzonga.
Baada
ya wabunge hao kumzonga, Profesa Kapuya ambaye amewahi kuwa waziri
serikalini alihoji kitendo cha mbunge huyo kupinga bajeti... “Kwa nini
umekataa kuunga mkono hoja? Ulikuwa unalidanganya Bunge wakati
unachangia si kweli huko Rukwa hakuna barabara, barabara mnazo.”
Kessy
alionekana kukerwa na swali hilo na kumjibu kwa hasira: “Nyinyi na
mimi nani ni mbunge Nkasi? Mimi sina unafiki napinga kutokana na
yaliyopo jimboni kwangu sipo hapa bungeni kuwafurahisha nyinyi na wala
Serikali. Nipo kwa masilahi ya wananchi wangu.”
Baada ya majibu hayo,
mbunge huyo aliondoka haraka eneo hilo. Baadaye
jioni mwandishi wetu alimfuata ili kupata ufafanuzi juu ya msimamo
wake.“Hakuna barabara kwangu, kwa nini niunge mkono hoja? Namshangaa
sana Kapuya kwa tabia aliyonionyesha pale... Mbona mama Margaret Sitta
amesema Tabora hakuna barabara hawakumfuata ?.”
Alisema
wabunge hao hawana haki ya kuhoji kwa nini hakuunga mkono hoja kwa
kuwa kila mmoja amekuja bungeni kutokana na kushinda katika jimbo lake. Akichangia hotuba ya bajeti hiyo, Kessy alisema haungi mkono hoja kwa
asilimia 100 hadi pale atakapoelezwa lini barabara hizo zitajengwa.
Alisema
zaidi ya vijiji 30 vya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Barabara ya
Kipili hadi Bandarini ni mbovu kwa kiasi kikubwa na muda wake wa ujenzi
kumalizika umeshapitiliza miezi mitatu iliyopangwa.
Alisema
nchi imegawanyika kwani baadhi ya majimbo ya wabunge yana lami hadi
mlangoni lakini Nkasi hawajawahi kuiona akitoa mfano wa Jimbo la Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki) Same Mashariki kwa Anna
Kilango.