Cindy ni kipaji kilichogunduliwa na producer Lamar. Ni rapper mrembo mwenye uwezo mkubwa tofauti na rappers wengine wote wa kike uliowahi kuwahamu Tanzania. Tofauti na wengine ni kuwa rap ya Cindy ina ladha ya kimataifa sana na licha ya kuwa mrembo anaweza kubadilika na kukaza kwenye mashairi hadi umsahau.
“I am a simple girl, kinda down to earth kidogo and I really have a big passion for rap,” anasema Cindy.”
“I used to be a singer, background vocalist, nimefanya nyimbo kibao za zamani lakini sikutaka jina langu lihusishwe. Baadaye nilipokuwa nasikiliza watu kama akina Fid Q, Nicki Minaj, Gosby, waliniinspire a lot and I was like ‘I have something more’ yaani kwanini tu niwe muimbaji halafu wasichana wengi ni waimbaji,” anaongeza.
“Halafu kuwa unafanya hizo rap na nini sio lazima uwe mgumu, I don’t have kudress ile kitomboy sababu siko hivyo. Bongo tumezoea kwamba female rappers ndo wanakuwa wagumu na nini, naweza nikaonekana mlaini lakini bado nikaandika mistari migumu kuliko hata wanaojifanya wagumu.”
“Kama unanifuatilia sasa hivi, nimebadilika kidogo and I’m enjoying the music I am making sasa hivi kwasababu ninaweza nikarelate nayo kweli katika maisha yangu ya sasa hivi.”
Cindy anafahamika pia kwa kuwa girlfriend wa rapper wa B’Hits, Gosby.
“Nilikutana naye wakati niko shule actually, alikuwa anasoma na mimi nilikuwa nasoma kipindi hicho hata nilikuwa sijaanza muziki, nilikuwa sifahamu kama na yeye yupo kwenye music, mara ya kwanza alinificha, yeah Gosby I know you seeing this!! Alinificha kwamba he is in the music industry na nini lakini that’s the first time I met him,” anasema Cindy.
Cindy anasema mazingira ya Tanzania kwa wasanii wa kike wanaofanya hip hop ni magumu na ndio maana wasichana ni wachache.
“Honestly ni magumu, mwanzoni ndio I heard hivyo kwamba ‘I can really do this yaani it’s really gonna be easy, I have what it takes, I have a good image labda, I believe in myself lakini nilivyoingia, I was like hiki sio kitu nilichoimagine kabisa!! Kwanza kabisa unapeleka nyimbo, unampelekea mtu CD yako, unamwambia kwamba ‘hii ngoma yangu labda nimeifanya sehemu fulani’ anakuangalia kwanza, anakuambia, ‘okay kwahiyo umeimba eeh’ yaani hata hakuulizi genre gani ya muziki unafanya, unamwambia like ‘ narap’ ‘ohhn unarap wewe’ unaju zile yaani mtu anakuanzia hapo halafu like ‘poa ntaisikia’ I think hiyo ni one of the reasons zinawakatisha tamaa wasichana.



