
Waumini wa kanisa la Kianglikana la Watakatifu wote la Mjini
Sumbawanga
Jimbo la Rukwa limelaani kitendo cha Askofu wao MhashamuMathayo
Kasagala kufungua kesi mahakamani akidai kukabidhiwa mali yakanisa hilo
ambalo waumini wake wamekataa kumtambua kuwa ni kiongoziwao tangia
alipochaguliwa kushika wadhifa huo miaka mitatu sasa.
Kufunguliwa
kwa kesi hiyo Rufaa No.1 ya mwaka 2013 ilyofunguliwa Aprili 15
inatokana na mgogoro wa muda mrefu ambao chanzo chakekiliotokana na
uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara .
Kasagara
ambaye aliIbuka mshindi kwa mujibu wa kura zilizopigwaviongozi wa
kanisa hilo katika uchaguzi wa mwaka 2010 huku baadhi yawaumini wa
kanisa hilo kiuhusisha ushindi wake na tuhuma ya vitendovya rushwa ili
kupata nafasi hiyo ambapo waumini kanisa la Watakatifu wote walijitenga
na kuchagua Kamati maalumu ya kuongoza kanisa hilo.
Akizungumza
kwenye kikao kilichofanyika Jumapili kwenye Mwenyekiti wakamati hiyo
Fulgence Rusunzu alisema kuwa baada ya kupokea samansi ya kesi hiyo
wameamua kukutana na kujadili kwa kina nini wakifanyekutokana mgogoro
huo kuonekana kuwa unanawiri upya.
Alisema
kuwa awali kamati yake ilifungua kesi ya kumzuia Askofu huyo kuingia
kanisani humo lakini baadaye waliamua kuiondoa kesi hiyo mahakamani
kutokana na maelekezo ya nyumba ya maaskofu ambao walizitaka pande zote
mbili kukaa chini na kuzimaliza tofauti zao nje
ya mahakama.
“Sisi
tumeshangazwa na Askafu Kasagara ambaye mwanzo aliafiki muafaka
upatikane kwa mazungumzo lakini hii leo anarejea mahakamani na kutaka
ukabidhi mali za kanisa, hivi lipi ni la muhimu waumini au mali za
kanisa" Alihoji Rusunzu.
Mmoja
wa waumini wa kanisa hilo Vicent Simba alisema kuwa waumini wa
Kanisahilo hawawezi kukubali kuongozwa na Kasagara kutokana na kukosa
mani naye katika uadilifu wake kiongozi.
“Hata
ndoa inapofungwa kanisani lazima wanandoa waulizwe iwapo anaafiki
kuona katika mkataba wan do hiyo, hivyo hakuna ulazima wa kiongozi
yoyote wa dini au serikali kuwashinikiza wamini wa kanisa hilo kukubali kuongozwa na Askofu huyo na ni bora wakaachwa wajiongoze
wenyewe”. Alisema Simba.
Akichangia katika kikao hicho Anna Chinolo alisema kuwa ni bora
wakajitenga na jimbo la Rukwa kuliko kulazimishwa kuwa kwenye jimbo mbalo linaongozwa na Askofu huyo.
“Kwani
jamani hivi sasa si tunapata huduma ya neon la Mungu kutoka kwa
watumishi wa Mungu tulio nao, je kuna haja gani ya kulazimishwa na
mtu, sisi hatutaki, watuache tuendelea kama tulivyo, tumekuwa watulivu lakini hizi kesi zinataka kutuvuruga tukose amani” Alisema
Chinolo
Mmoja wa Wachungaji wa kanisa hilo Elisafani Ndijenyene aliwataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuacha
kumfikiria Askofu huyo pekee.
Katika
mazungumzo ya awali ya Askofu Kasagara ambaye aliwahi kufika wenye
kanisa la Watakatifu wote la mjini Sumbawanga na Januari 23 waka 2011 na
kuishia kukaa nje ambapo alisema kuwa anaaminilichaguliwa kihalali na waumini hao wanaomkataa ni wale waliokengeuka
.
“Mimi Kasagara naamini kuwa hawa wamekengeuka tu lakini ipo siku
watakaa chini na kutafakari hatimaye watarudi kuwa watu wangu baada ya
kupata nuru ya Mwenyezi Mungu.” Alisema Kasagara.