Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 30, 2013

Upelelezi vurugu za Lema Uhasibu wakamilika


MBUNGE wa Jimbo la Arusha Godbless Lema (aliyevaa kombati nyeusi) anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali Julai 2 mwaka huu baada ya upelelezi wa kesi yake kukamilika. Lema anakabiliwa na kesi ya uchochezi, kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani katika Chuo cha Uhasibu Njiro, Arusha. Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Eliainenyi Njiro aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Msofe, Njiro aliiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe ya kusoma maelezo ya awali ya mtuhumiwa.

Naye Wakili Humphrey Mtui anayemwakilisha Lema aliiomba Mahakama kupanga muda wa mbele baada ya Juni 28, Mwaka huu ili mteja wake amalize vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Kutokana na mapendekezo hayo Hakimu Mkazi Msofe alikubaliana na maombi hayo na kupanga shauri huilo hadi Julai 2 mwaka huu.

Mtuhumiwa Lema anadaiwa kati ya Aprili 24, Mwaka huu kutenda kufanya uchochezi,kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani kinyume na kifungu cha 390 na kifungu cha 35 cha Sheria ya makosa ya jinai sura namba 16, marejeo ya 2002.

Akiwa katika Chuo cha Uhasibu (IAA) Aprili 24, mwaka huu, Lema anadaiwa kutamka maneno yaliyosababisha uvunjifu wa amani.

Maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mbunge huyo ni “Mkuu wa Mkoa anakuja kama anakwenda kwenye send off na hajui mahali chuo hicho kilipo na alishindwa kuwapa pole wanafunzi hao kwa kufiwa na mwanafunzi mwenzenu.

Mengine ni “Mkuu huyo hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu pamoja na kuwa hakuwasaidia kutokana na matatizo yao.”

MTANZANIA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...