ZAIDI ya asilimia 75 ya Watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi wanajihusisha katika sekta isiyo rasmi.
Kauli
hiyo imetolewa kutokana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini
kuzidi kushika kasi hali inayoendelea kuzitesa nchi za Afrika Mashariki
na za kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kazi na Ajira katika Wizara ya Kazi na Ajira, Ally Msangi
alikuwa akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali
kujadili hali ya soko la ajira duniani.
Msangi alisema utafiti utakaofanywa utagusa sehemu kubwa ya nguvu kazi
na utaiwezesha serikali kupata picha halisi ya hali ya ajira nchini.
Utafiti huo utatoa taarifa kuhusu hali ya ajira nchini katika sekta
isiyo rasmi, utumikishwaji wa watoto, hali ya hifadhi ya jamii, hali ya
kipato nchini na matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika
sekta zote kwa kipindi cha 2006-2013.
“Katika kufikia dira ya maendeleo ya taifa (Vision 2025) Tanzania
imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwamo kukuza uchumi na kupunguza
umaskini Tanzania (MKUKUTA) wenye malengo ya kuhakikisha kiwango cha
ukosefu wa ajira kinapungua, utumikishwaji wa watoto unapungua na ajira
isiyo timilifu inapungua.
“Utafiti huu pekee wa hali ya nguvu kazi nchini ndiyo unaweza kutoa hali
halisi ya viashiria hivyo ili kufikia malengo na maendeleo
tunayoyahitaji,” alisema Msangi.
Alisema imebaki miaka miwili kufikia hitimisho la tathmini ya malengo ya
maendeleo ya millenia (MDGs) mwaka 2015 ambako nchi inapaswa kutoa
taarifa ya viwango vya viashiria vya malengo hayo hususani katika MDGs.
“Wote ni wadau nuhimu katika mchakato huu kwa kuwa masuala ya ajira na
kazi ni masuala mtambuka ambayo juhudi za pamoja zinahitajika kati ya
serikali,t aasisi za elimu, taasisi za utafiti ,wawekezaji, mashirika
yasiyo ya serikali,w abia wa maendeleo,waandishi wa habari na wananchi
kwa ujumla ili kufikia malengo tuliyojiwekea,”alisema Msangi.