Jeshi
la Polisi nchini limesema tukio la mlipuko wa Bomu lililotokea jijini
Arusha hivi karibuni na katika maeneo mengine ya ukanda wa nchi za
kusini mwa Afrika ni mingoni mwa matukio ambayo yanafanya ukanda huu
kuwa katika hatari zaidi ya kukabiliwa na matishio ya kigaidi na kuahidi
kuchukua hatua zaidi za kudhibiti hali hiyo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP SAID MWEMA amebainisha hayo mara baada ya kufungua mkutano wa Kimataifa wa Wakurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai wa nchi za Kusini mwa Afrika, ambapo ameongeza kuwa majeshi ya Polisi ya nchi hizo kwa kushirikiana na vikosi vya INTERPOL yatajadili mpango mkakati wa kudhibiti matukio hayo pamoja na matukio mengine yanayohatarisha hali ya Usalama.