Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige,
ndiye aliyeanzisha mjadala asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu,
baada ya kumuuliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
kuhusu mpango wa serikali kudhibiti ukahaba.
Magige
aliuliza kuhusu fikra za serikali juu ya mpango wa kupeleka muswada
bungeni, kuhusu uundwaji wa sheria ya kudhibiti ukahaba nchini.
Swali
hilo la Magige, lilikwenda sambamba na maelezo kuwa biashara ya ukahaba
inavyoshamiri, inazidi kusababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Alisema,
biashara hiyo vilevile ni kichocheo cha kushamiri kwa maambukizi ya
Virusi Vya Ukimwi, kuongezeka kwa watoto wa mitaani na kukua kwa uhalifu
kwa sababu kuna uporaji hufanyika kwa kuwatumia hao wanaojiuza.
Akijibu
swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,
Sophia Simba, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema
serikali inajitahidi kuimaliza biashara ya ukahaba nchini.
Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Aliongeza kuwa serikali inatumia taasisi mbalimbali za kijamii kuielimisha jamii kuhusu athari za ukahaba.
Magige,
aliuliza maswali mawili ya nyongeza, moja akitaka kutungwa kwa adhabu
kali, maana zile zitolewazo sasa zimeonekana ni dhaifu, pili akataka
takwimu ya kesi za ukahaba ambazo zimesharipotiwa mpaka sasa.
Akijibu
maswali hayo, Kairuki alisema kuwa umuhimu wa kutoa adhabu kali ni
mkubwa lakini akasema tatizo ni jamii, kwani imekuwa ikiyajua madanguro
ya makahaba lakini watu hawatoi ushirikiano.
Kuhusu
takwimu, Kairuki alisema kuwa mwaka jana, ndani ya Jiji la Dar es
Salaam, kesi 22 ziliripotiwa Mahakama ya Jiji na watuhumiwa 123
walihukumiwa.
Wakati
huohuo, baadhi ya machangu wameliambia Amani kuwa watakuwa wakitembea na
tindikali kama nyenzo ya kujilinda wanapokuwa katika shughuli zao.