Ujumbe
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) uko nchini Rwanda kubadilishana
ujuzi na uzoefu na Rwanda kuhusu utekelezaji wa mradi wa kurahisisha na
kuwezesha biashara (Trade Facilitation) kwa kutumia TEHAMA – Electronic
Single Window System.
Muda mfupi ujao TPA itaanza utekelezaji wa mradi
huo kwa niaba ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji, Forodha,
wafanyaniashara na wadau wote wa Tanzania.
Ujumbe huo wa Tanzania unaongozwa na Mkuu wa mradi na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya TEHAMA-TPA Ndg. Phares Magesa wa kwanza kushoto katika picha juu, wengine ni Mathayo Ntandu, Jesse Shali na Kilian Chale ambao ni maofisa wakuu TPA.



