Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyani amethibitishwa kukamatwa
kwa Tapeli huyo na kwamba kwa sasa alikuwa akifanya kazi kama Project
Cordinator wa Agape Foundationi Asasi isiyo ya kiserikali
inayoshughulikia masuala ya Watoto Yatima wilayani Njombe.
Kamanda
Ngonyani amesema Mtuhumiwa Huyo kama Jina lake Linavyojieleza kwenye
Tangazo na Picha Zake mwenye umri wa Miaka 27 Mkazi wa SIDO Njombe
amekamatwa Jana majira ya Jioni hivyo hatua za kumsafirisha kupelekwa
makao makuu ya Polisi Jijini Dar es Salaam zinaendelea kutokana na kesi
yake kufunguliwa Huko.Aidha amesema kuwa hadi sasa wanamsubiri Askari atakayetumwa toka Makao makuu Jijini DAR Kuja kumchukua.
Taarifa za awali zilieleza kutafutwa kwa Tapeli huyo toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.INAPOTOKA
: Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013, tuliripoti kupitia
blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini kuhusu kuwepo kwa
mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia jina la taasisi
yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya huruma kwa
masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa Zoom
Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza
nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya
Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo
aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na
kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa wamepata
nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka wamtumie
shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa
kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA
JINA LA RAFIKIELIMU )..
Baada
ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza
kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja kati yao
akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu mara baada ya
kutembelewa na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo. Dada
huyo aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni
Muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika
ofisi zetu siku ya tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili
asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya kufanya naye mazungumzo
ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao fanyika kwa jina
la taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda kuripoti uhalifu huu
kwenye kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es
salaam, na kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA
MTANDAO.
Hashim Mkane, tapeli anayetafutwa kwa kosa la Kutapeli mtandaoni kwa jina la RafikiElimu. |
Mara
baada ya kupata RB moja kwa moja tulipost taarifa ya
kuwatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa mtu anaye tapeli
watu kwa kutumia jina la taasisi yetu, huku tukiwaachia polisi
na kazi ya uchunguzi wa tukio hili la uhalifu. Wakati polisi
wakiwa bado wanaendelea na uchunguzi, siku ya Jumatatu ya
jana, tarehe 11 Machi 2013 saa sita kamili asubuhi, tulipokea
simu kutoka kwa mwakilishi wetu wa Mwanza, Dada HADIJA SEJA
akiomba tumpe namba za " MR. EMMANUEL ALBERT " ( HR wa
RafikiElimu Foundation ).. Kwa kuwa tayari tulikuwa na taarifa
za jina hilo, tulimuomba dada Hadija Seja atutaarifu kitu gani
kimetokea. Dada Hadija alitupa taarifa ya kusikitisha sana,
kwamba kuna mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja tu la Gerlad
kutoka Arusha, amewasili jijini Mwanza kuripoti katika ofisi za
taasisi ya RESTLESS DEVELOPMENT kwa ajili ya kuanza kazi. Mtu
huyo naye ni muhanga wa tapeli huyu, na baada ya kumtumia
tapeli huyo sh. elfu tano, tapeli alimuagiza aende kuripoti
jijini Mwanza katika ofisi za RESTLESS DEVELOPMENT ( mabazo
kimsingi hazipo Mwanza ). Can You imagine, huu ni unyama wa
kiwango gani, kumfanyia masikini mwenzako ushenzi kama huo?.
Baada
ya kupata taarifa hii, moja kwa moja tukaamua sisi wenyewe
kama taasisi kwenda katika ofisi za VODACOM makao makuu
zilizopo Mlimani City ili kuweza kumbaini mtu anaye fanya
unyama huu...
Tunashukuru sana Mungu, Vodacom walitupa ushirikiano wa
kutosha.. Kutoka kwenye database za Vodacom, tuligundua kwamba,
mtumiaji wa 0763906931 anaishi Njombe. Namba hii imesajiliwa
MPESA tarehe 02 February 2013, hakusajili kwa kitambulisho chake
halisi, bali kwa barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za
Mitaa. Alisajili akiwa NJOMBE na alipokea simu nyingi sana.
Zaidi ya watu kumi waliingia katika mkenge wake na kumtumia
hizo shilingi Elfu Tano.
Mwanzoni
alikuwa ana toa hela zake kwa wakala ambaye alisajilia namba
hii, lakini baadaye alisafiri na kwenda tarafa nyingine hivyo
basi kushindwa kutoa hela kwa sababu namba ameisajili kwa
jina ambalo sio lake. Hivyo basi ili kuweza kutoa pesa
ilimbidi, ajihamishie salio kutoka katika namba 076390631 kwenda
kwenye namba yake halisi ambayo ni 0765283703. Hapo ndipo
tulipo weza kumbaini tapeli huyu.
Jina la huyu mtu anaitwa HASHIM MKANE na namba yake halisi
ni 0765283703. Ni mkaazi wa Njombe na amehitimu Chuo Kikuu
Cha Sokoine ( SUA ) . Aliwahi kuomba nafasi ya uwakala wa
RafikiElimu katika wilaya ya Njombe, mwezi Agosti 2012.
Baada
ya kupata taarifa hizi tuliamua kutafuta mbinu za kumkamata
kirahisi,ambapo tulimtumia barua pepe, jana jioni kisha ujumbe
mfupi wa maneno ( SMS ) tukimwambia aje Dar Es salaam
kuhudhuria semina ya siku tano ya mawakala wa RafikiElimu (
Tukamtajia na malipo ). Nadhani alistukia kwamba huenda
ameshajulikana, akatuma ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka :
"
Nashukuru kwa taarifa hii ingawa nitashindwa kuhudhuria kwa
kuwa taarifa imechelewa kufika na ukichukulia mimi ni
mwajiliwa wa taasisi binafsi hivyo kuweza kupata ruhusa kwa
siku moja au mbili ilihali tunafanya evaluation ya mradi ni
ngumu. natumai kuhudhuria semina nyingine kama mtaiandaa "
Hapa
tukajua jamaa ameshastukia mchezo na uwezekano wa kumkamata
kwa njia hiyo usingekuwa rahisi. Hivyo basi tumeamua kuweka
taarifa hii mtandaoni pamoja na picha za mtuhumiwa huyu, ili
kwa yoyote yule atakaye fanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu
aweze kupewa zawadi nono ya shilingi Laki Tano za kitanzania
. Taarifa nyingine zitatumwa kwenye magazeti na televisheni ili
iwe rahisi kusambaza ujumbe kwa watanzania wengi na hivyo
kurahisisha kutiwa hatiani kwa dhalimu huyu . Tafadhali upatapo
ujumbe huu, wafahamishe na ndugu jamaa na marafiki zako
woote...
UKIMUONA MTU HUYU, TOA TAARIFA KATIKA KITUO CHOCHOTE CHA
POLISI KILICHO KARIBU NAWE , KISHA WASILIANA NASI KWA SIMU
0782405936. NA ENDAPO TAARIFA YAKO ITASAIDIA KUKAMATWA KWA
TAPELI HUYU, TUTAKUPATIA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU ZA KITANZANIA
SHILINGI LAKI TANO ( Tsh. 500,000/ =)..
Hashim Mkane, mwenye namba 0765283703 tapeli wa mtandaoni, aliyewatapeli makumi ya wananchi kwa jina la RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia kazi katika taasisi mbalimbali. |
(
KWA TAMAA YA PESA KIDOGO, AMEJIDHALILISHA, AMEDHALILISHA TAALUMA
YAKE, AMEDHALILISHA CHUO CHAKE, AMEWADHALILISHA WAZAZI, WAKE, NDUGU ,
JAMAA NA MARAFIKI ZAKE, KWELI WAHENGA WALISEMA TAMAA ILIMPONZA
FISI NA MCHUMA JANGA , HUCHUMA NA WA KWAO. )
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe limewataka wananchi kufanya kazi kwa uaminifu bila udanganyifu