Viongozi wa ngazi za juu nchini Kenya, wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta na
Makamu wake William Ruto, ni miongoni mwa waliopendekezwa kushtakiwa
katika ripoti ya kushtusha iliyotolewa na Tume ya TJRC.
Kutoka mjini Nairobi Sudi Mnette amezungumza na Profesa Ezebio Wanyama
ambaye pamoja kuwa mwanasheria wa kimataifa pia ni mchambuzi katika
medani ya kisiasa alejikita katika masuala ya ICC. Kwanza alitaka kujua
umuhimu wa ripoti hiyo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya
spika za masikioni hapo chini.