Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Ney Wamitego amesema Nikki Mbishi na
wasanii wengi wachanga huwa wanajaribu kuwa-diss wasanii wakubwa kwa
lengo la kupata jina.
Ney alizungumza hayo pale nilipotaka kujua kutoka kwake juu ya kitendo
cha msanii Nikki Mbishi kutengeneza wimbo unaoitwa Ney Wamitego, wimbo
ambao unaonekana moja kwa moja unamzungumzia Ney Wamitego kama mwanamke
au mwanaume siyo.
Mwanzoni mwa mazungumzo yangu nilitaka kujua kutoka kwa Ney,
anachukuliaje kitendo cha msanii huyo kuandika wimbo unaomzungumzia
yeye, Ney alikataa kuzugumza hilo huku akisema "Yaani kaka mimi
nikiongea kitu tu mimi nampa kick ile anayotaka yule dogo, mi sitakiwi
kuongea kitu, yaani hiki ndio kitu ambacho watu wa karibu wamekuja
wameniambia this time huyu amefanya hiki kwa sababu ya hiki, so dont
talk anything"