Thursday, May 30, 2013
Msichana ajitokeza na kudai kuwa Justin Bieber ni baba wa mwanae mwenye miaka miwili!
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 27 amejitokeza na kudai kwamba staa mdogo mwenye matukio makubwa Justin Bieber alimpa ujauzito baada ya kufanya naye mapenzi tarehe 4 February 2010.
Chanzo kimoja kimeliambia jarida la Star kuwa msichana huyo alijifungua mtoto wa kike mwezi October 2010 baada ya kuwa na usiku wa pamoja na Bieber huko Miami Beach February 4, 2010 aliyekuwa akiperform siku hiyo.
Chanzo hicho kiliendelea kusema sababu za msichana huyo kutomwambia Bieber ambaye mwaka (2010) alikuwa na miaka 15, kuhusiana na mtoto huyo anayedai kuwa ni wake, ni kuwa alitaka kumlinda mwanae na familia yake kwa kutotaka kuwa kwenye spotlight.
Kwa mujibu wa jarida hilo, msichana huyo ambaye hajataka jina lake litajwe amesema anahitaji Justin Bieber ajue kuwa yeye ni baba wa mtoto wa kike wa miaka miwili, lakini hatahitaji pesa yoyote kutoka kwake na wala haitaji kuwa sehemu ya maisha ya ustaa wa baba wa mtoto wake.
Msichana huyo ambaye wakati anakutana na Bieber (kama anavyodai) alikuwa na miaka 25, aliongeza kuwa anamuachia maamuzi yote Justin Bieber mwenyewe kama atakuja kuhitaji kujihusisha kwa namna yoyote na mwanae baadae au laa.
Je wewe unaamini kuwa Bieber anaweza wa kuwa baba wa mtoto wa miaka miwili?