MSANII
wa filamu nchini Tanzania Rose Ndauka azidi kujizolea umaarufu na
kuongeza mashabiki wa aina zote kwa kuwa karibu na watoto wa mitaani
hususani katika matembezi yake ya kila siku
Akizungumza jijini Dar es
Salaam Ndauka alisema kuwa katika maisha yake hususani kwa kipindi hiki
ambacho yeye ni supar staa anathamini watoto wa aina yote kwani hao ndio
moja ya mashabiki wake
Alisema kuwa anawathamini
watoto hao hali inayomsababisha kutembea kwa miguu ili kila anapokutana
nao apate nafasi ya kuzungumza nao na kubadilishana nao mawazo kwa
kufanya hili anaamini kuwa anaongeza mashabiki wake na kuwafanya watoto
hao kuwa karibu nao
Ndauka ambaye anaamini watoto
wa mitaani wanahitaji upendo wa kila mmoja anayemzunguka alisema kuwa ni
jukumu lake na nafsi yake inamsukuma kufanya hivyo ili kuzidisha upendo
na kuwafanya wahisi ni sehemu moja ya jamii
Aliongezea kuwa kila
anapokutana na watoto hao anahisi faraja moyoni mwake kwani hiyo ni
sehemu ya kitu anachokipenda na nyakati za siku ya mapumziko hutumia
muda wake mwingi kutembea kwa ajili ya kuwaona watoto na kupata mawazo
yao ambayo anayatumia katika kuboresha filamu zake




