MBUNGE wa
Kigoma Kaskazini Zitto (Chadema) Kabwe ameonyesha nia ya kupinga ama
kuikwamisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kutokana na
hatua ya Serikali kugawa vitalu vipya kabla ya kuwepo kwa sera na sheria
mpya ya madini.
Taarifa
za ndani kutoka kwa watu wa karibu na Mbunge huyo zinadai kwamba mbunge
huyo anajiandaa kuandaa utaratibu wa kupinga bajeti hiyo mpaka serikali
itakapo leta sheria mpya, “Serikali imegawa nakala za bajeti ya Nishati
na Madini na wabunge wote wanatakiwa kuhudhuria semina hiyo, lakini
chakushangaza ni kwamba nakala zote zimeandikwa kwa lugha ya
Kiingereza"kilisema chanzo hicho.
Mbali na
mtoa taarifa hiyo kudokeza Habarimpya.com juu ya suala hilo Mbunge huyo
pia aliandika taarifa za kikao hicho katika ukurasa wake wa Facebook na
kudai kwamba hatua hiyo ya serikali inapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
"Kati ya
Wabunge waliopinga hatua hiyo ni pamoja na Zitto Kabwe ambaye alisema
kwamba Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na tayari imetangaza tena kugawa
vitalu vya mafuta na gesi kaskazini mwa Ziwa Tanganyika.endelea kupitia na kukopi audifacejackson blog."Haraka
hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi?
Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha
maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa kwa vizazi vya sasa na
vijavyo"alisema Zitto na kuongeza:
"Uamuzi
wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo kwa sera na sheria mpya
unapaswa kupingwa kwa nguvu zote.kwani inabidi tuangalie ni wapi
tunakwenda na kwa manufaa gani baadae sio tu tuwe tunakimbilia posho".