
Kwa kawaida mapenzi hutawaliwa na hisia za kimahaba
alizonazo mtu kwa mwenziwe ama mtu anaetamani kuwa nae kama
boyfriend/girlfriend wake ama mke/wake. Lakini hakukosea aliyesema mapenzi ni
kama mmea unaweza kutunzwa na kustawi na ukiachwa bila matunzo unaweza
kunyauka.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo Karrueche Tran aliyetoswa
vibaya na Chris Brown lakini kwa kuweka mikakati ya dhati na kuumwagilizia
vyema mmea wa penzi kati yake na na Chris hata wakati akiwa hana muda nae na
anahang out na Rihanna kumemsaidia kurudisha kwa kasi na nguvu mpya penzi
alilopoteza.
Moja kati ya mikakati ya kimahaba aliyoitumia Karrueche huku moyoni mwake akiuamini msemo wa ‘mvumilivu hula mbivu’, ni kujiweka karibu na Chris kama rafiki hata wakati akiwa bado yuko na Rihanna na hakuonesha chuki ya wazi kwake japokuwa alikuwa anaumia sana.
Mkakati mwingine ni kuhakikisha anaonesha moyo wa upendo wa
dhati na nia ya kuwa na Chris Brown kwa kuwa alijua kabisa kuwa mwisho wa siku
ataangalia zaidi anakooneshwa kupendwa na kuvumiliwa, akijua mwisho wa siku
akiumizwa na kulizwa huko aliko atahitaji kufutwa machozi na kutulizwa, na
Karrueche atakuwa karibu zaidi, na kweli ndicho kilichotokea.
Chanzo cha karibu na KT kimesema, “Karrueche hakuwahi kuacha
kumpenda Chris, hakuwa kulazimisha kitu chochote kwake kwa upande wa mahusiano,
na hakuwahi kulazimisha kupewa kitu mkononi au kuomba chochote kwake.”
Mkakati huo pia ulimuongezea alama za ushindi kwa jamaa,
lakini pia alijua kabisa ya Rihanna yatapita tena, kwa imani yamepita kweli.
“Alijua alikuwa bado anafanya vyote na Rihanna na alitegemea hilo na muda wote
alikuwa rafiki kwa Chris Breezy hata wakati akiwa na Rihanna.” Kiliendelea
kufunguka chanzo hicho.