Makala na Denis Mtima na Chande Abdallah /GPL.
Ripoti
ya Wiki hii imegundua kuwa asilimia kubwa ya mayai yanayotumiwa na
wananchi wengi kwa sasa ni feki na yanauzwa kinyemela ndani ya Jiji la
Dar.
Baada ya
kupigwa vita na serikali miezi michache iliyopita, imebainika kuwa bado
yamezagaa na watu wanaotajwa kuyatumia kwa kiasi kikubwa ni wauza
chipsi mitaani.
Mayai
hayo ambayo hayatofautiani na mayai ya kuku wa kizungu yaliyozoeleka kwa
kuwa na muonekano wa rangi nyeupe sana, imebainika kuwa yanatengenezwa
kwa kutumia mashine maalum za umeme.
Ili
kubaini uwepo wa mayai hayo ambayo serikali kupitia Bodi ya Chakula na
Dawa (TFDA), iliwatahadharisha wananchi kutotumia kwa madai kuwa yana
madhara kiafya, cha kushangaza bado yamezagaa mitaani kama njugu.
Ripoti
ya Wiki imejaribu kufanya utafiti wa kina na kugundua uwepo wa mayai
hayo hasa katika maeneo ya Buguruni na Sinza, Dar ambapo ilidaiwa kuwa
mzigo mkubwa wa mayai hayo ulitokea nchini Kenya.
Aidha,
kuanza kuuzwa tena kwa mayai hayo siku za hivi karibuni, kunatokana na
wakazi wa jiji kutojali aina ya vyakula wanavyokula, jambo linalotoa
mwanya kwa wachuuzi hao kuyapenyeza mayai hayo kwa siri kwenye mzunguko
wa mayai ya kawaida.
Ripoti
ya Wiki ilizungumza na mmoja wa wauza chipsi waliokutwa na mayai hayo
ambaye alikiri uwepo wa mayai hayo na kubainisha kuwa yanasambazwa na
wauzaji wakubwa ambao wanasemekana kuwa waliyanunua kwa wingi kabla
serikali haijayapiga marufuku.
“Haya
mayai mbona yapo mengi tu. Sinza nzima, ukiuliza unayapata. Watu wengi
wanayakataa. Ambao hawayajui tunawabambikizia wanakula,” alisema muuza
chipsi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.