MAHAKAMA
kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imepinga vikali taarifa ya jeshi la
polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda aliyoitoa jana kwa
vyombo vya habari kuwa inamshikilia mtumishi wa mahakama hiyo kwa
kuiba bangi iliyofikishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
"Taarifa
ya kamanda wa polisi kuwa bangi imeibiwa mahakamani si ya kweli na
imelenga kuichafua mahakama. Mahakama hawajapata kuibiwa. Taarifa hizo
si za kweli kabisa".
Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake kaimu msajili wa
mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya alisema mahakama
inasikitishwa taarifa ya Jeshi la polisi inayoupotosha umma kwa kutoa
taarifa ya
uongo bila kufanya uchunguzi.
Amesema kungekuwamo kuibwa vielelezo, ilipaswa kuwepo kwa mlalamikaji ambaye ni Mahakama kwenda kufungua kesi polisi.
Tunakanusha
vikali kuwepo kwa upotevu wa kielelezo cha bangi katika mahakama hii
Exhitibit Room haijavunjwa iko intact... tulikuwa na kielelezo P.3
katika shauri hilo la jinai namba 24/2012 ambayo ni bangi viroba 8
amri ya mahakama ya kuteketeza ilitolewa tarehe 13/2/2013 na bangi hiyo
iliteketezwa chini ya uangalizi wa afisa wa jeshi la polisi na kesi
hiyo ilikwisha tarehe 13 /2/2013 na mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha
miaka miwili jela.".Endelea kupitia audifacejackson blog..Alisema
kama ilivyokuwa katika kesi nyingine za jinai, “tunatoa wito kwa jeshi
la polisi Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuona bangi hiyo imepatikana
wapi kwa kuwa sisi hatuhusiki.”.Endelea kupitia audifacejackson blog..Pia
alisema kama kweli mahakama kuna vielelezo vilivyoibwa, basi polisi
wangefika kufanya upelelezi hata kuwahoji kama njia ya kuchunguzi .
"Tunalishauri jeshi la polisi kufanya utafiti wa kina kuhusu suala hili kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari"