MWANAMUZIKI
Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia
kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. ...
Katika
hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds
Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. ...
Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.
Jaydee
aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya
saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama
hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo...
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la
Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe
wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe
alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka
kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
Kati ya vielelezo alivyopewa
na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na
nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets!
Taarifa za mwanadada huyo
kufikishwa mahakamani hapo, ziliibuka chinichini kwenye mitandao ya
kijamii, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baadaye Lady Jaydee alihoji
kuwa pengine yeye ndiye anayestahili ‘kukinukisha’ kwa kuwapeleka
mahakamani wasanii walio chini ya Tanzania House of Talent (THT),
Estarlina Sanga ‘Linah’ na Elias Barnaba ambao anadai aliwalipa kianzio
cha shoo yake ya Mei 31, mwaka huu kisha kumchomolea dakika za mwisho