DIVA
wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper, ameonekana
kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia kitendo cha yeye
kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia na sasa
amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline WolperAkizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya
huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa atakayempa
nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye sana
kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki
yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo
sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka
pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki
itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu
wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu
hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”
Source:Global publisher




