Hatimaye hali ya afya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini, Robert Manumba(Pichani juu), imeimarika na amerejea kazini, limeandika Mwananchi Akizungumza kwa njia ya simu, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alikiri kuwa Manumba amereje kazi ingawa hakuwa tayari kutaja tarehe aliyoingia kazini.“ Eh! Unauliza nini, mbona ameanza kazi siku nyingi, siwezi kukumbuka tarehe sipo ofisini naelekea kwenye kikao cha kazi,” alisema Senso.Habari za kuaminika kutoka kwa baadhi ya maofisa wa kitengo cha upelelezi, zilisema kiongozi huyo ameshaanza kazi baada ya afya yake kutengemaa.Manumba mwenyewe, kifupi alisema “Kwa sasa sijambo, ninakwenda kwenye mkutano.” Mkurugenzi huyo alirejea nchini April 22, mwaka huu akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Millpark.