Kalapina kulia akiwa na fan wake
Baada ya muasisi wa harakati za hip
hop Tanzania Kalapina kumchapa Rapper Chidi Benz katika jukwaa la maisha
club alfajiri , Kalapina ameelezea sababu za kutoa dozi hiyo kwa msanii
mwenzake, namnukuu " ukweli
ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au heroin / unga
anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane
na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake utakua m'baya,mimi
nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda jukwaani nikawa naskia
sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama nane, alikua
ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu mtu si adui,
nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata na kumpa
dozi, siku akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu, hakuna
hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete
ukimharibia utaishia jela."