
Vurugu
hizo zilisababishwa na baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanapinga
kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ambapo
walifanya uharibifu wa miundominu mbalimbali ikiwemo kuchoma nyumba
zaAskari Polisi.
Akizungumza
katika kikao cha Maofisa na Askari polisi mkoani hapa Kamishna Chagonja
alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema amesikitishishwa
sana na vitendo vya uchomaji wa nyumba hizo na amewataka kutovunjika
moyo katika kufanya kazi.
Alisema
kilichowapata Askari hao ni changamoto katika kazi na wanapaswa
kuzikabili ili kuhakikisha wanaendelea kulinda usalama wa raia na mali
zao na raia wachache wasiopenda amani wanakamatwa na kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
“Raia
wema ni wengi na wahalifu ni wachache hivyo lazima tuhakikishe wale
wote wanaofadhili na kuhamasisha vurugu hapa mkoani mtwara tunawakamata
na kuwafikisha mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa kuwa
vitendo wanavyovifanya sio vizuri hasa kuchoma makazi ya watu”Alisema
Chagonja.
Wakati
huohuo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Mohamed
Kodi amesema katika kipindi chote cha vurugu zilizotokea mkoani hapa
hakuna mgonjwa yeyote aliyefika hospittalini hapo na kulalamika
kufanyiwa vitendo vya ubakaji kama taarifa zilivyoenea katika vyombo
mbalimbali vya habari.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi
Linus Sinzumwa alisema mpaka hivi sasa hawajapokea malalamiko yoyote
kuhusiana na vitendo hivyo na amewataka kama wapo watu waliofanyiwa
vitendo hivyo wapeleke malalamiko yao katika kamati iliyoundwa
inayojumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
“Naomba
malalamiko hayo yawe ya msingi na siyo ya uzushi na uongo na pindi
ikigundulika kuwa maneno hayo ni ya uzushi na uongo sheria itachukua
mkondo wake dhidi ya wahusika” Alisema Sinzumwa.
Amewataka
wakazi wa Mtwara kuendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu na
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili wahusika wote wa
vurugu hizo waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.