|
Choo cha msupastaa wetu, kikionyesha ilipokuwa TV |
|
Choo cha Rihanna |
Baada ya Rihanna na masupasta wenzie kuwa na mtindo wa
kuweka TV chooni na kupiga picha kuonyesha nyumba zao kwa wapenzi na wafuasi wao hatimae mtindo huo washika kasi
kubwa katika masupastaa wa hapa Bongoni. Kile kipengele cha kuweka TV chooni
kimepelekea supersta wa Bongoni kutaka kupoteza uhai wake baada ya
kuweka TV ya Mchina chooni, na bahati mbaya ilikuwa na matatizo hivyo basi
wakati msupa staa akiwa anajisaidia, (Mjumbe wa serikali ya mtaa amesema alikuwa anakata gogo), akawa anabadilibadili chaneli,
bahati mbaya akapigwa shoti na kulazimika kukatisha ile shughuli na kutimkia
nje, nguo magotini. Bahati mbaya sana mwandishi wa hii blog isiyo na maana na ukweli mchache
kabisa hasa hizi siku za kikao cha Bunge,alikuwa anapita akawahi kupiga picha
ya choo hicho ikionyesha sehemu ambapo msupastaa alijenga ili kuweka TV yake ya
Mchina.
|
Inasemekana ni msupastaa baada ya tukio |
Hata hivyo blog hii inapongeza maendeleo makubwa yanayoonyeshwa na
masupastaa wetu kufikia hatua ya kuweka vitu kama TV, friji, geskuka, friza,
oven na kadhalika chooni, kama vilevile wanavyofanyaga akina Jel o na Rihanna