BAADA YA SINTAH......NISHA NAYE AOGOPA KUMTANGAZA MPENZI WAKE KWA KUHOFI MABINTI WA MJINI:
Katika kile kinachoonekana kama mwendelezo ama tabia za wanawake
kuibiana wapenzi hasa hawa wenye majina makubwa nchini, mwigizaji wa
bongo movies Salma Jabu al maarufu kama Nisha, naye amegoma kumtaja
mpenzi wake hadharani kwa madai ya kuwa anaogopa kunyang'anywa tena
mpenzi wake huyo kama ilivyotokea alipokuwa na mpenzi wake wa zamani
"Nay wa Mitego''-msanii maarufu wa bongo fleva nchini amabye naye
kipindi cha nyuma likuwa mwigizaji.
Akiongea na gazeti moja
maarufu la udaku nchini, Nisha amesema kuwa amejifunza kwa yaliyomtokea
na sasa yupo mwangalifu sana na penzi lake, kwani anajua kina dada hawa
hawatasita kufanya lolote ili mradi wakuchukulie mpenzi wako na kukuona
ukiahangaika.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa msanii wa bongo
movies kufanya kitendo kama hiki baada ya mwanadada Sintah naye kuamua
kumficha mpenzi wake.