Wanafunzi
wa shule ya serikali ya Mzumbe Sekondari jana saa nane usiku
wameandamana kutoka shueleni kwao wakieleke ofisi ya mkuu wa mkoa
wakishinikiza serikali ya mkoa wa Morogoro kuwatimua walimu wao watano
akiwemo mkuu wa shule hiyo wakiwashutumu kwa vitendo mbali mbali ikiwemo
vya ufisadi.Wanafunzi
hao walizuiwa na askari eneo la Mindu saa 12 alfaji ya na kwamba kwa
umoja wao madent hao waligoma kutoka barabnara mpka mkuu wa mkoa au
katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro kufika kwenye eneo hilo na kusikia
kilio chao.
Katibu
Tawala wa mkoa huo Bw.Elias Ntandu kwa kushirikiana na Afisa Elimu wa
mkoa wa Morogoro Bi Wariambora Nkya na viongozi mbali mbali wa
halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mvomero ilipo shule hiyo waliufika
kwenye eneo la Mindu na kusikiza malalamiko ya wanafunzi
hao.Akizungumza kwa niaba ya wenzeke kiongozi wa wanafunzi hao Bw Emily
Mayani aliueleza uongozi huo wa serikali ya mkoa kwamba hawata rudi
shule mapka serikali itakapo watimu walimu watano akiwemo mkuu wa shule
hiyo Bw Dismas Njawa.na msaidizi wake Bw Mtalasi.
Walimu
wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mwalimu wa malezi wa
shule hiyo Edwin Matenga,mwalimu wa nidhamu Mohamed Soni na mwalimu wa
taaluma Gasbert Rwegasira,kwa mujibu wa wanafunzi hao hao walimu hao
waliowaita Top 5 wanawashutumu kwa mambo mbali mbali ikiwemo ya ufisadi
na lugha za matusi kwa wanafunzi.
Viongozi
wetu michango jambo moja kuwafukuza mara moja walimu hao kutufukuza
sisi wanafunzi 60 ambao asilimi 90 wazazi wetu ni wakulima mfano mimi
wazazi wangu ni wakulima wa nyanya,hatuwezi kuvumilia uongozi unatumia
shilingi milioni 50 kupaka rangi chumba kimoja tukio hoji tunaambia sisi
watoto wadogo na kwamba kama tunataka twenda kukasoma shule ya
wasichana ya kilakala hayo si matusi makubwa, mbali na ufisadi huo baa
imejengwa eneo la shule yetu wakati sheria za nchi zinatuzuia wanafunzi
kukaa au kuingia baa"alisema kiongozi huyo wa wanafuzni wa shule hiyo
kwa jazba kubwa.
Uongozi wa serikali hiyo ya mkoa uliwaomba wanafunzi hao kuwa watulivu na kuahdi kuyafanya kazi mapendekezo hayo waliyotoa