MCHEZA
sinema mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka
kuwa kila aingiapo kwenye kazi ya kurekodi filamu, anapatwa na tatizo
la kupandisha maruhani, jambo linalomkosesha raha.
Akizungumza
na Exclusive Star, Batuli alisema kuwa hapendi kumhisi vibaya mtu
yeyote juu ya tatizo hilo lakini hali hiyo inamkosesha amani kwani
haelewi chanzo cha tatizo lake ni nini.
“Mimi
kwa kweli sitaki kabisa kuweka imani tofauti ya kumhisi mtu vibaya ila
najiuliza kwa nini nipandishe maruhani wakati wa kurekodi peke
yake?” alisema Batuli.
Batuli
aliongeza kuwa kinachomchosha zaidi hata akienda hospitali, huwa
haonekani kama ana tatizo lolote, hali ambayo inampa mawazo zaidi.
“Namuomba Mungu anisaidie kwa maana
hata tatizo lenyewe hospitali halionekani, inanitisha kweli,”alisema Batuli.