MSANII
wa filamu ambaye alikuwa Muislam na baadaye kuamua kuingia kwenye
Ukristo na kuokoka, Ruth Suka ‘Mainda’ sasa anaonekana kupambana vilivyo
kuhakikisha anaiboresha imani yake kwa kutembea na Biblia kila
anakoenda.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Mainda aliyeomba hifadhi
ya jina lake alisema kuwa msanii huyo anaonekana kuwa na uchu wa kuijua
vilivyo Biblia.
“Kwa
kweli sasa hivi Mainda hakaukiwi na Biblia mkononi, yeye na Biblia kila
wakati. Kuna wakati hata akiwa lokesheni, akipata muda kidogo anaitoa
na kuanza kuipitia. Hakika amebadilika,” kilisema chanzo hicho huku
maneno hayo yakishibishwa na picha alizotupia Mainda kwenye mtandao wake
wa Facebook zikimuonesha akiwa ameshikilia kitabu hicho kitakatifu.