MSANII
mkongwe wa muziki wa bongo fleva ambaye mpaka sasa anashikilia taji la
mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba
juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya
kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada
ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa
kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo
bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao
kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.
Afande
Sele alipohojiwa na arushaone blog alidai kwamba Kilio hicho
kilitokana na maudhui ya wimbo huo ambao ulimkumbusha mambo mengi"
Nikweli nimeshindwa kujizuia na kuangua kilio nilipokuwa na imba wimbo
wa Mkuki Moyoni,kiukweli wimbo ule ulinikumbusha jambo moja ambalo
stoweza kulitaja kwa sasa"alisema Afande Sele baba wa watoto wawili
Tunda na Asantesanaa
Cheka akipanda jukwaani kumbembeleza rafiki yake kipenzi..Aidha
baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya rafiki mkubwa wa Afande Sele
bondi Francis Cheka'SMG' alipanda jukwaani na kubembeleza msanii huyo
ambaye baada ya kubembezwa na Cheka alikubali kunyamaza kwa mashariti ya
kutoendelea kuimba wimbo huo wa Mkuki Moyo ulioombwa na mashabiki
wengi.Badala yake aliimba wimbo
wa Darubini kali ambao alishirikiana kuimba na bondia Cheka aliyemudu
vyema nafasi ya kiitikio iliyoimbwa na mdogo Dito na Mc Koba ambao kwa
sasa wametengana na msanii huyo na kuunda kundi lao la watu
Poli ,Cheka alikamua ile ile hali iliyoongeza radha ya burudani kwenye
wimbo huo
Baada ya Cheka kufanikiwa kumtuliza Afande Sele waliimba wote wimbo wa Darubini Kali
Cheka na Sele wakikamua kwenye shoo shoo
NA DUSTAN SHEKIDELE