Mfanyabiashara Apolnary Malamsha (33) wa Arusha ambaye jicho lake
limepata hitilafu baada ya kutobolewa na chuma cha bomu wiki mbili
zilizopita akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jana. Picha na Beatrice
Moses
“Nimechunguzwa na daktari ameniambia kwamba kipande cha chuma
kilichotoboa jicho langu kiliingia ndani na kukata mojawapo ya mishipa
inayowezesha jicho kuona kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuona tena,”
alisema kwa masikitiko Malamsha.
Malamsha pia anasumbuliwa na kutapika, hali ambayo anadai inachangiwa na vyuma vya mabomu vilivyoingia mwilini mwake.
Naye kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la Priscus Malamsha ambaye
alikuwa akimhudumia alieleza kuhuzunishwa na habari hizo kwa kuwa
inaweza kumpunguzia mdogo wake furaha ya maisha yake.
“Najisikia vibaya huyu ni mdogo wangu, lakini bomu limemfanya apoteze
furaha yake, tazama anavyotapika kila anachokula, lakini tutaendelea
kumtazama Mungu,” alisema Malamsha ambaye naye ni mkazi wa Olasiti.
Kijana huyo ni miongoni mwa majeruhi saba waliofikishwa MNH kwa
matibabu zaidi, baada ya kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea
katika Kanisa Katoliki la Mtakafitu Joseph Mfanyakazi.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa MNH, Jeza Waziri alieleza kuwa
majeruhi karibu wote wanaendelea vyema,baadhi yao wanaweza kuruhusiwa
kurejea nyumbani kwao hasa kutokana na hali zao kuendelea kuimarika.
Majeruhi wengine ni Gabriel Godfery (9), Jenipher Joachim (40) na Anastazia Regnard (14).
Wengine ni Albert Njau (35), Faustine Shirima (33) Fatuma Tarimo (38)
ambaye amepimwa na kuonekana ana chembechembe za vyuma vya bomu ndani
ya tumbo lake.
credit- Gazeti -mwananchi