Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha
Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO.
Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.
Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya
ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.
Nanukuu "Lengo la
hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye
uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao
kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona
mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea
uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa
mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi
kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK)
kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora
kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante
sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"