Mkuu
wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akizungumza kwenye kilele cha
maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yaliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya Mandewa mjini Singida.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida,waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Diwani
wa viti maalum (CCM) manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akitoa burudani
na mzee Juma Ntandu kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za muungano
wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa
Singida mjini.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Serikali
ya wilaya ya Singida, imewaagiza wakazi wake kuimarisha ushirikiano na
jeshi la polisi,ili kulinda kikamilifu amani na utulivu ulioasisiwa na
muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu
wa wilaya hiyo, Queen Mlozi ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye
kilele cha maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, zilizofanyika kiwilaya katika viwanja vya Mandewa Singida
mjini.
Amesema ili tuweze kutekeleza ipasavyo shughuli zetu za kiuchumi na kijamii,tunahitaji sana hali ya amani na utulivu.
“Ili
tuweze kudumisha amani na utulivu uliopo,kila raia mwema ni lazima awe
askari wa mwenzake na tuwe wepesi kutoa taarifa kwa viongozi au vyombo
vya usalama kila tunapomtilia mashaka mtu ye yote”amefafanua Mlozi.
Katika
hatua nyingine,mkuu huyo wa wilaya,aliwataka wakulima kuacha tabia ya
kuuza mazao wakiwa shambani ambayo yananunuliwa kwa bei ndogo mno.
“Niwakumbushe
kuwa tuache kabisa tabia ya kuuzia mazao shambani tena kwa bei ya
chini.Musimu wa kuvuna baadhi ya mazao ya chakula umeanza,tusisahau
kuweka akiba na kutumia vizuri chakula ulichopata,ili tujikinge na
njaa.Ni aibu kwa Wanasingida kuomba chakula”,amesema.
Mlozi
amesema kuwa wilaya katika msimu huu wa masika, umepata mvua za kutosha
hivyo hategemei kupata taarifa za wananchi kuomba chakula mwaka huu wa
2013, labda itokee sababu maalum za msingi.
Aidha,
Mlozi amesema mafanikio yaliyopatikana kupitia muungano huu wa
Tanganyika na Zanzibar,hatuna budi kuyasdumisha kwa kufanya kazi halali
kwa juhudi na maarifa.
Mkuu
wa Wilaya hiyo amesema “Muungano wa Tanzania ni lazima ubaki kuwa ni
kiashiria cha muungano miongoni mwetu wananchi.Ni lazima tuoneshe
muungano katika shughuli za maendeleo baina ya mtu na mtu, taasisi moja
na nyingine, wananchi na serikali yao”.